Klabu ya Simba yamtimua Robertinho

Klabu ya Simba SC imeachana na kocha wao Robert Oliveira ‘Robertinho’ baada ya makubaliano ya pande zote mbili kwa maana ya klabu na mhusika. 

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia mitandao ya kijamii imeeleza kuwa pia wamefikia makubaliano ya kuachana kocha wa viungo Corneille Hategekimana. – 

Aidha imesema katika kipindi hiki cha mpito timu itaongozwa na kocha Daniel Cadena akisaidiwa na Suleiman Matola.