Korea Kaskazini leo imerusha kiasi cha kombora moja la masafa marefu kuelekea eneo la baharini.
Hatua hiyo imetajwa kuwa huenda inaongeza juhudi zake za kufanya majaribio ya makombora yake ambayo yanaweza kufuatiwa na hatua ya kurushwa kwa kombora lenye uwezo wa kuvuka mabara.
Mkuu wa majeshi nchini Korea Kusini hakusema mara moja ikiwa silaha hizo zimehusika kwenye jaribio hilo la kurusha makombora au ni kwa umbali gani kombora hilo limekwenda.
Hata hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu wa Japan katika wizara ya ulinzi imesema hatua hiyo huenda imehusisha kombora la masafa marefu wakati jeshi lake la ulinzi wa pwani likitoa tahadhari kwa vyombo vya majini vinavyopita karibu na eneo hilo la bahari.