Mratibu wa zoezi la sensa kitaifa Seif Kuchengo anasema kuwa zoezi hilo hilo linaendelea vizuri ambapo amesema kuwa kuna dodoso maalumu ambalo linatutumika kwa kaya ambazo wahusika hawatokuwa nyumbani kipindi makarani watakapopita
Kupitia dodoso hilo karani utaweza kufuatilia tarifa za kaya kwa ukaribu zaidi
Pia ametoa wito kwa wanaoiba vifaa vya kutendea kazi za sensa waache mara moja kwa kuwa vifaa hivyo ni mali ya serikali na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watakao bainika kuiba vifaa hivyo.
Kwa mujibu wa Kuchengo, siku ya kwanza ya sensa wamehesabu kwa asilimia 15.45,ambapo kaya zilizohesabiwa ni milioni 2.35, watu milioni 10.26 na katika idadi hiyo wanaume ni asilimia 48.3 na wanawake ni asilimia 51.7
.