Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru, amefariki dunia leo Novemba 9,2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India.
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelezea kupokea kwa masikitiko kufuatia kifo cha Mchumi huyo ambaye amewahi kuhudumu katika taasisi kubwa za umma na binafsi.
“Ninatoa pole kwa Familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Watumishi wa Tume ya Mipango, Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia msiba huu”
“Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali, Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema, Amina” – Rais Samia
Mafuru alikuwa Mchumi maarufu nchini kutokana na taaluma yake ya fedha ambapo aliweza pia kuhudumu kama Msajili wa Hazina na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NBC Tanzania.
Mbali na nafasi hizo aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki nchini (TBA) na Mwanzilishi Mwenza wa Kampuni ya Masuala ya Ushauri wa Fedha ya Bankable