Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), kimefungua shauri katika Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar se salaam dhidi ya Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania pamoja na Mwanasheria Mkuu wa wa Tanzania kuhusu kanuni zinazosimamia tozo nchini humo.
Hivi sasa mjadala mkubwa nchini Tanzania ni kuhusu ongezeko la tozo ambalo licha ya serikali kuahidi kufanyia kazi ongezeko hilo lakini bado limekuwa maumivu kwa wananchi wa kipato kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.
Katika shauri hilo namba 42 la mwaka 2022 LHRC, inaomba Mahakama iruhusu kituo hicho kuwasilisha maombi ya kufanya mapitio ya kimahakama(Judicial Review ili kutengua kanuni hizo kwa kuwa zilitungwa bila kufuata utaratibu ulioanishwa ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kuhusu upitushwaji wa tozo kwa njia ya kielektroniki.
Aidha LHRC inaomba mahakama kuweka zuio la muda la kuendelea kutumika kwa kanuni hizo hadi pale kesi ya msingi itakapofikia mwisho.