Lissu aongoza matokeo uchaguzi wa Chadema, Mbowe akubali

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wameamua kubadili upepo  baada ya kumchagua Tundu Lissu kuongoza Jahazi akiwa kama Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

Licha ya kuwa hakujatangazwa matokeo ya jumla lakini matokeo  yanaonyesha ushindi wa Lissu dhidi ya wapinzani wake Freeman Mbowe na Odero Odero.

Lissu anakuwa Mwenyekiti wa nne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, akitanguliwa na Edwin Mtei, Bob Makami na Freeman Mbowe ambaye anamuachia kijiti Lissu baada ya kuhudumu kwa miaka 21.

Uchaguzi wa Chadema umekuwa na mvuto kwa kufatiliwa na wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania huku wengi wakitoa maoni yao wakisema kwamba Chadema imekomaa kisiasa