Imeelezwa kuwa jumla ya madereva bodaboda 759 wamefariki dunia kutokana na ajali za barabarani kati ya mwaka 2022 na 2024.
Akitoa takwimu hizo leo bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, mbali na vifo vya madereva hao, Sillo amesema kuwa wananchi wa kawaida 283 pia wamefariki dunia kutokana na ajali za bodaboda katika kipindi hicho.
Aidha kwa upande wa wananchi waliokuwa wanatembea kwa miguu, kandokando ya barabara au njiani ama walikua wanavuka barabara na kupata ajali ya kugonongwa na pikipiki na kufariki dunia ni 71.
Sillo amewataka madereva wa pikipiki kuzingatia sheria za barabarani ikiwemo kutopakia abiria zaidi ya mmoja lengo likiwa ni kupunguza vifo nchini.