Mahakama ya Afrika Mashariki imetupilia mbali ombi la kutaka kusimamisha ujenzi wa bomba la mafuta ghafi lenye thamani ya $4bn (£3.1bn) kutoka Uganda hadi nchini Tanzania.
Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ) jana Jumatano iliamua kwamba kesi hiyo iliwasilishwa kwa kuchelewa na kwa hivyo ilizuiliwa kwa muda na nje ya uwezo wake.
Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Eacop) lenye urefu wa kilomita 1,443 (maili 896) linalojengwa na serikali ya Uganda na Tanzania pamoja na TotalEnergies na China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) limekabiliwa na msukumo mkubwa kutoka kwa wanaharakati wa Mazingira wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu haki na mazingira. .
Makundi hayo yanasema kuwa mradi huo unawahamisha wanajamii kutoka katika ardhi yao, unadharau makaburi kando ya njia ya bomba na kusababisha madhara ya kimazingira.
“Hukumu hii inaashiria muendelezo wa jinsi gani kaskazini mwa dunia na taasisi mbalimbali za serikali barani Afrika hazioni uharibifu wa mazingira na athari za mafuta na gesi katika hali ya hewa,” shirika la kiraia la Natural Justice lilisema katika taarifa yake.
Natural Justice na mashirika mengine matatu ya kiraia ambayo yaliwasilisha kesi hiyo mwaka wa 2020 walisema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.