Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Majaliwa:Serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu uhifadhi katika eneo la Loliondo - Mwanzo TV

Majaliwa:Serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu uhifadhi katika eneo la Loliondo

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Kassim wa Tanzania.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu suala la uhifadhi katika eneo la Loliondo lililopo kwenye wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

 “Katika mjadala wetu wa leo(jana), mmetoa maoni nasi tumeyapokea. Bado Serikali inayaangalia maslahi mapana ya umma. Tutawashirikisha pia ni lipi lina maslahi mapana kwa Watanzania.”

 Ametoa kauli hiyo leo (Jana Februari 14, 2022) wakati akizungumza na wadau wa uhifadhi kwenye kikao kilichofanyika Wasso-Loliondo. Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea maoni waliyoyatoa, yatayojumuishwa na kuyawasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan. 

 Majaliwa alifika Loliondo jana ikiwa ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa na wabunge kwa Serikali kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Utalii iliyoielekeza Serikali iende katika maeneo ya Loliondo, Ngorongoro na Sale kuzungumza na wananchi.

 “Kama ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza lazima tuimarishe utalii na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa, Waheshimiwa wabunge ambao ndio wawakilishi wametoa maoni yao ikiwemo kushauri suala la ushirikishwaji na ndio maana leo nimekuja hapa kuwasikiliza”.

Amesema kuwa inaeleweka kuwa idadi ya watu na mifugo imeongezeka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro hivyo suluhusho linahitajika kwa haraka kukabiliana na hali hiyo kwani endapo hapatakuwa na suluhu ya haraka hifadhi hiyo zitaathirika. 

“Sisi sote tunatambua eneo hili ni la utalii, lazima tufike mahali tuamue kama tunataka utalii au la,” amesema na kuongeza

“Sote tunatambua kuwa ardhi iliyo ndani ya mipaka ya nchi hii ni ya umma lakini tumeikasimu kwa Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Katika kikao hicho, wananchi wa makundi mbalimbali walipewa nafasi kutoa maoni yao wakiwemo mbunge, madiwani, malaigwanan, wanamije (batemi) na wenyeviti wa vijiji. 

Katika maoni yao, wengi wao walisema wako tayari kushirikiana na Serikali kuendelea kutunza rasilimali za Taifa.