Search
Close this search box.
Africa

Majeruhi saba Kati ya 15 waliokuwa wamelazwa hospital ya Rufaa ya Mkoa Ligula, wamepewa rufaa kwenda hospitali nyingine kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Ligula, Dk. Clemence Haule, amesema majeruhi watatu kati ya hao saba wamepelekwa Muhimbili na wengine wanne wamepelekwa hospital ya Rufaa Ndanda.

Amesema jana walipokea majeruhi 18, ambapo watatu walipoteza maisha wakati wakiendelea  na matibabu.

“Kati ya hao 15 walikuwa wanaendelea vizuri, isipokuwa hao watano tuliwaandikia Rufaa wakatibiwe sehemu nyingine,” amesema kuongeza kuwa baadae leo asubuhi waliongezeka wagonjwa 2 na kufanya idadi kuwa 7.

Amesema wengine waliobaki wanane wanaendelea vizuri na hali zao zinazidi kuimarika.

Ajali hiyo ilitokea jana Julai 26 ambapo watu 13 walifariki akiwemo dereva wa gari hilo pamoja na mama mmoja ambaye aliomba lifti katika gari hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gari kufeli breki na hivyo kusababisha kupoteza uelekeo na kuingia kwenye shimo.

Comments are closed