Majira ya saa nne asubuhi Paul Makonda anawasili Ofisi ndogo ya makao makuu ya CCM yaliyopo Lumumba akiwa kwenye msafara wa bodaboda na kupokewa na umati wa wafuasi na viongozi wa chama na Serikali.
Makonda amewasili akiwa kwenye bodaboda kwa kile kilichodaiwa kuwa alishindwa kufika na gari lake kutokana na msongamano wa magari na umati wa watu uliojitokeza kwenye eneo la ofisi hiyo.
Mara tu baada ya kuwasili katika ofisi hizo, Makonda alikabidhiwa ofisi na mtangulizi wake ambaye ni Sophia Mjema kwa sasa ni Mshauri wa Rais mauala ya Wanawake, Watoto na Makundi maalum tukio lililofanyika kabla ya kuongea na vyombo vya habari.
Katika tukio hilo, Sophia amesema kitengo hicho ni moyo unaotegemewa na chama hicho kuhakikisha katika chaguzi zinazokuja kinapata ushindi wa kishindo.
“Nimehudumu kwenye nafasi hii kwa kipindi cha miezi tisa nilikabidhiwa kijiti na Shaka Hamdu Shaka na juzi Oktoba 22 Chama kilifanya uteuzi na leo nakukabidhi wewe, tunaimani kubwa utatimiza azma ya chama chetu,” amesema.
Amesema anafahamu kwa kuwa wote kwa muda mrefu walikuwa huko serikalini lakini amekuja kukitumikia chama ambacho shabaha yake ni kuendelea kushika dola.
“Una timu kubwa ya kushirikiana nayo, nawaomba watumishi ninaowaacha mpeni ushirikiano dhabiti katika muendelezo wa kukijenga chama chetu,” amesema.
Makonda anena
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema kuteuliwa kushika nafasi hiyo ni kwa mapenzi ya Mungu aliyemfungulia milango akiomba ampe hekima, busara na uvumilivu kukitumikia chama hicho tawala kwa uadilifu.
“Sina maneno mengi nasema asante sana kwa kuwa mtumishi wa wengi, ni matumaini yangu mlango ambao Mungu ameufungua atanipa hekima, busara na uvumilivu na kukitumikia chama kwa uadilifu, uaminifu na mafanikio makubwa ili nisimuabishe Mungu wala Rais aliyeniamini na kuniteua katika nafasi hii,” amesema Makonda.
Akiwahutubia mamia ya wanachama waliofia kwa ajili ya kumpokea Makonda ametumia fursa hiyo kuwaomba watumishi wenzake wa chama hicho kumpa Ushirikiano na kumshauri.
“Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa zinafanya uamuzi, ukiwa na chanzo kibovu utafanya uamuzi mbovu, lakini ukiwa na chanzo kizuri utafanya uamuzi sahihi wakati wote,” amesema Makonda akisisitiza kuwa ushirikiano utakifanya CCM kuendelea kuwa na mashiko kwa wananchi.
Pamoja na hayo Makonda amasema tangu ateuliwe kuna Watu wamehamaki wengi wao wakiwaza kuwa Makonda ataenda kulipa kisasi huku wengine wakiwataja baadhi ya Watu na kuwaambia âUtaona sasa usiyemtaka kajaâ, ambapo Makonda amesema hajaja kulipa kisasi kwa yeyote.
âTangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupitapita kwenye mitandao, nimesoma maoni ya baadhi ya Watu, wengi wanahamaki na wengi wana bashasha lakini wanaohamaki wengi wao wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi, nimeona na wengine wanaanza kuwataja Watu wengine kwamba âUtaona sasa usiyemtaka kajaâ, naomba niseme Mimi sina kisasi kwa Mtu yoyote.
âNa asiwepo Mtu yoyote yule akafikiri lengo langu ni kumkandamiza, au nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikiri wamenitenda mabayaâ âMnaohisi kuna jambo halikuwa sawa Mimi naelewa Mungu aliwatumia kunisaidia kumjua Mungu zaidi, naamini Mungu aliwatumia ili kuniandaa kwa kazi kubwa zaidi msiwe na hofu, naomba ushirikiano na umoja wenu na wala Dkt. Samia hajaniteua kuja kuhangaika na mambo ya Makonda bali uenezi wa CCM na wala Dkt. Samia na Kamati Kuu haikukaa kwenye kikao kumtafuta Mtu wa kwenda kulipa kisasi, walimtafuta Mtu atakayeongeza nguvu katika kujenga imani ya Watanzania kwenye CCMâ
Awapa tahadhari Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Watendaji wa Serikali na vyama vya upinzani
Katika hotuba yake hii leo ambayo imetumia zaidi ya dakika 20 Makonda ametoa angalizo kwa viongozi wakiwemo mawaziri wote, wakuu wa mikoa na watendaji wote kwamba chama hicho hakitosita kuwachukulia hatua endapo watabainika kuwa hawajafanya kazi zao kikamilifu.
Amesema chama hicho ni sikio la Serikali na sauti ya wananchi, hivyo kazi yao ni kusikiliza kwa niaba ya serikali na kusema kero na matatizo ya wananchi kwa niaba yao.
âSitakuwa tayari kuwa msemaji wa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi, na wanaomsaidia mheshimiwa mwenyekiti wanashindwa kutekeleza nisimame hadharani kusema uongo, hapana. Kila kiongozi wa serikali atabeba msalaba wake mwenyewe,â amesema.
Aidha, amewakosoa wanaotaka muungano wa Tanzania uvunjike ili wapate nafasi ya kuingia madarakani akituma salamu kwao kuwa vijana na watoto wote waliozaliwa ndani ya muungano hawako tayari kuwa historia ya wao kuuharibu muungano huo.
Mbali na hayo, amesema chama hicho kupitia mwenyekiti Rais Samia Suluhu kimejitosheleza kwa hoja, hivyo anatoa salamu kwa jeshi la polisi kuruhusu vibali na ulinzi kwa vyama vya upinzani, huku akiiomba mamlaka ya anga kumpa kibali cha kuruka na helikopta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kufanya ziara zake, kwa kuwa chama hicho hakitegemei kufanya figisu zozote kutokana na uwezo na utekelezaji wa ilani usio wa mashaka.
Ameenda mbali zaidi akisema kwamba kwa sasa Tanzania haina chama cha upinzani, Tanzania ina vyama vya watoa taarifa waliojikusanya kwa jina la vyama.
âTanzania haina chama cha upinzani, Tanzania ina vyama vya watoa taarifa waliojikusanya kwa jina la vyama. Ukimuona Tundu Lissu anaongea sio taarifa ya Chama, ni mtu anatoa taarifa na wakati mwingine taarifa anazotoa zimetoka kwenye chanzo sio sahihiâ amesema Makonda