Search
Close this search box.
East Africa

Indaiwa kuwa takriban watalii 1,000 wa Ukraine wamekwama katika visiwa vya Zanzibar vilivyo nchini Tanzania baada ya anga ya Ukraine kufungwa kwa safari za ndege za kiraia kufuatia hatua ya kijeshi ya Urusi nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Shirika la Habari la BBC NEWS, Serikali ya Zanzibar imesema inawasiliana na ubalozi wa Ukraine katika nchi jirani ya Kenya ili kuwahamisha watalii hao hadi Poland.

Waziri wa utalii visiwani Zanzibar  Leila Mohammed Musa alisema usalama na ustawi wa watalii unazingatiwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya hoteli ambazo watalii wanakaa zimepunguza bei zao, huku zingine zikitoa malazi ya bure kwa wageni ambao wamekaa zaidi.

Mandhari ya pwani ya Zanzibar na utamaduni wa kihistoria ni kivutio kikubwa kwa watalii wa kigeni.

Mmoja wa watalii hao aliambia BBC kwamba walikuwa wakifuatilia matukio nchini Ukrain kutoka kwenye hoteli zao.

Ukraine ilifunga anga yake wiki iliyopita ikitaja hatari kubwa ya usalama wa ndege kutokana na matumizi ya silaha na zana za kijeshi.

Comments are closed