Search
Close this search box.
Africa

Mawakili wa Serikali wakwamisha kesi ya CHADEMA

11

Mahakama Kuu, Masijala ya Dodoma, imeahirisha usikilizwaji wa kesi ya Chadema dhidi ya Jeshi la Polisi baada ya Mawakili wa Jamhuri kutofika Mahakamani. 

Chadema, ilifungua shauri hilo jana kuiomba Mahakama itoe amri kwa Jeshi la Polisi kumfikisha mahakamani au kumuacha kwa dhamana Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza la Vijana (Bavicha), Twaha Mwaipaya.

Kesi hiyo iliyopo mbele ya Jaji Adam Mambi imeahirishwa leo Jumanne, tarehe 5 Julai 2022, hadi Jumatatu ijayo ya tarehe 11 Julai 2022.

Wakili wa Mwaipaya, Fred Kalonga amedai baada ya upande wa Jamhuri kutotokea mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa maombi hayo, licha ya kupewa wito wa mahakama, walimuomba Jaji Mambo kesi iahirishwe hadi kesho, lakini alikataa ombi hilo akisema atakuwa safarini.

Wakili huyo amedai, mteja wake anayeshikiliwa na Polisi tangu akamatwe tarehe 30 Juni 2022, hakufikishwa mahakamani hapo.

“Maombi yalipangwa mbele ya Jaji Mambo, tumewapeleka wito wa mahakama jamhuri kwa maana ya IGP, RPC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini hakukuwa na upande wowote waliokuja mahakamani. Ikawa busara ya jaji kutoendelea na maombi hayo sababu upande mmoja haupo,” amedai Wakili Kalonga na kuongeza:

“Tukamuomba tuahirishe hadi kesho akatuambia anakwenda safari na tarehe atakayokuwepo ni Jumatatu.”

Comments are closed

Related Posts