Ugonjwa wa Ukimwi umekuwepo duniani sasa kwa takriban miaka 40 tangu ulipogunduliwa mara ya kwanza nchini Marekani. Kumekuwa na majanga mengine ambayo yamezuka na kupata chanjo kama vile UVIKO 19 lakini kupatikana kwa dawa thabiti au chanjo dhidi ya Ukimwi imekuwa safari ya muda mrefu.
Tangu 1981 hadi sasa Ugonjwa wa Ukimwi ulipozuka, bara la Afrika bado linaoongoza kwa idadi ya maambukizi mapya na idadi kubwa ya vifo. Makundi maalum yakiongoza katika maambukizi hayo mapya.
Ili kuelewa unyanyapaa na wakati mgumu ambao makundi haya hupitia katika kupiga vita janga la Ukimwi, Mwanahabari wa Mwanzo TV alifanya mahojiano na mwanaharakati wa makundi ya LGBTQ na watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi