Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Mfumuko wa bei wa Taifa wapungua  - Mwanzo TV

Mfumuko wa bei wa Taifa wapungua 

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari,2022 umepungua hadi asilimia 4.0% kutoka asilimia 4.2% kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 .

Kaimu Mkurugenzi Sensa ya watu na takwimu za jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi.Ruth Minja amesema hii ikimaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari ,2022 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba,2021.

Minja amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Januari ,2022 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Januari ,2022 ikilinganishwa na kipindi kilichoishia mwezi Disemba 2021 .

“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Januari ,2022 umepungua kwa asilimia 3.1% kutoka asilimia 3.9% kwa ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2021 huku mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula visivyochakatwa ,nishati na bili za maji [Core Inflation] kwa mwezi Januari 2022 umepungua hadi asilimia 3.3% kutoka asilimia 4.6% ilivyokuwa mwezi Disemba 2021.” amesema Minja

Aidha ,kaimu Mkurugenzi huyo ameainisha baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mavazi kutoka asilimia 4.5 hadi asilimia 2.8%,viatu kutoka asilimia 4.6% hadi asilimia 4.4%,kodi ya pango kutoka asilimia 4.4% asilimia 1.2%.magodoro kutoka asilimia 12.3%hadi asilimia 7.3%,majokofu kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 1.5%,cherehani kutoka asilimia 9.1% hadi asilimia 5.0%, simu janja kutoka asilimia 3.5 hadi asilimia 3.3%.

Vingine ni vyombo vya nyumbani kama sahani kutoka asilimia kutoka asilimia 16.7% hadi asilimia 3.6% ,luninga kutoka asilimia 3.5% hadi asilimia 1.2% na malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kutoka asilimia kutoka asilimia 6.6% hadi asilimia 2.9%.

Katika hatua nyingine Bi.Minja ameainisha mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo nchini Uganda umepungua hadi asilimia 2.7% kutoka asilimia 2.9 % huku nchini Kenya ukipungua pia kutoka asilimia 5.39 % kutoka asilimia 5.73.