Miaka sita tangu Tundu Lissu apigwe risasi

Leo imetimia miaka sita katika historia ya maisha ya mwanasiasa na mwanasheria nguli nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye sasa amepata ulemavu wa kudumu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana siku kama ya leo Septemba 7,2017 jijini Dodoma kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama  kikuu cha upinzani, Chadema alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu na hatimaye kwenda Ubelgiji kwa matibabu zaidi ambako alikaa kwa zaidi ya miaka mitatu 

Mwanasiasa huyo mwenye misimamo mikali ya kisiasa alirejea Tanzania mwaka 2020 na kuwania urais ambapo alishindwa dhidi ya Hayati John Magufuli aliyekuwa akiwania muhula wake wa pili kupitia chama tawala cha CCM.

Hata hivyo baada ya kushindwa uchaguzi huo aliodai kuwa ni uchafuzi na si uchaguzi kutokana na hujuma zilizofanywa na chama tawala ili kumuangusha, aliamua kurejea tena ubelgiji kuendelea na matibabu huku akiahidi kurejea nchini.

Na sasa Lissu yupo nchini rasmi huku akiendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya kuhakikishiwa usalama wake na Serikali ya Tanzania.

Hadi sasa hakuna taarifa ya mshukiwa aliyetekeleza shumbulio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu