Mke na Mume wadaiwa kumuua mtoto wao wa miaka 8

Paskari  Erinest(46) na mkewe Jeska Balitazali (39) wote wakazi wa Sengerema wanashikiliwa na  Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wao Aneth John(8) mwanafunzi wa darasa la awali shule ya Msingi Nyancheche.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Hamis Mwampelwa amedai moto huyo amepoteza maisha Machi 29, 2022 saa 11 jioni baada ya kupigwa na mama yake mzazi, Jeska Balitazali.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwampelwa amedai mama huyu alikuwa na desturi ya kumpiga mtoto huyo hadi kukimbia nyumba na kuhamia kwa majirani.

Mara baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.