MKUTANO WA SADC WAANZA LEO MALAWI

Southern African Development Community.

Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za SADC, umeanza leo nchini Malawi katika mji wa Lilongwe, ambapo unatarajia kumalizika kesho. Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali wa jumuiya hiyo, akiwemo Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi wakiongozwa na mwenyeji wao Rais wa Malawi Lazarus Chikwera.  

Kati ya mambo yatakayofanyika katika mkutano huo ni pamoja na kuithiboitisha Malawi kuwa mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja 2021/2022.Malawi inapokea kijiti cha nafasi hiyo kutoka kwa nchi ya Msumbiji ambayo nayo ilipokea kijiti hicho kutoka Tanzania, kama ulivyo utaratibu wa jumuiya hiyo kupewa nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaaka mmoja.