Baada ya miaka miwili janga la UVIKO-19 bado halijaisha na linaweza kukaa kwa muda mrefu zaidi kwa sababu ya usambazaji wa chanjo âusio sawaâ, katibu mkuu wa UN alionya Jumatano.
âAthari kubwa ya janga hili imekuwa kwa afya na maisha ya mamilioni, na zaidi ya visa milioni 446 vya maambukizi ya UVIKO 19 kote ulimwenguni.
Vifo zaidi ya milioni sita vimethibitishwa, na isitoshe watu wengi wamesalia kupambana na afya mbaya ya akili,â mkuu wa UN Antonio Guterres alisema katika taarifa yake huku janga hilo likifika mwaka mmoja tangu ligunduliwe.
âNafurahi kuwa hatua bora za afya zimechukuliwa, na usambazaji wa chanjo katika sehemu nyingi za ulimwengu zinadhibiti janga hili,â alisema.
âLakini itakuwa kosa kubwa kufikiria janga limekwisha.â
Guterres alibainisha kuwa âusambazaji wa chanjo unabakia kutokuwa sawa,â na kwamba wakati dozi bilioni 1.5 za chanjo zinatolewa kila mwezi, âkaribu watu bilioni tatu bado wanasubiri chanjo yao ya kwanza.â
âKushindwa kwa usambazaji sawa wa chanjo ni matokeo ya moja kwa moja ya maamuzi ya kisera na kibajeti ambayo yanatanguliza afya ya watu katika nchi tajiri kuliko afya ya watu wa nchi maskini,âalisema Guterres.
Taarifa hiyo ilihitimisha kwa kutoa wito kwa ulimwengu wote âkujitolea tena kumaliza janga hili … na kufunga sura hii ya kusikitisha katika historia ya wanadamu, kwa mara ya mwisho.