Mnyika: No Reforms No Elections Ilikua Chini Ya Mwenyekiti Mbowe

Shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, John Mnyika, ameendelea kuhojiwa kwa maswali ya dodoso na upande wa Jamhuri katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Mnyika: No Reforms No Elections Ilikua Chini Ya Mwenyekiti Mbowe

Mnyika, ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, amekuwa akijibu maswali ya Wakili wa Serikali Mkuu, Nasoro Katuga, kuhusu Katiba ya chama hicho, majukumu yake kama mtendaji mkuu, vyanzo vya fedha za chama pamoja na misingi ya kisiasa inayosimamiwa na CHADEMA.Katika sehemu nyingine ya maswali hayo, Katuga amemhoji Mnyika kuhusu mkutano wa CHADEMA wa Aprili 3, 2025, uliokuwa na kauli ya “No Reforms, No Elections”, ikiwemo nani aliyeandaa hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho na iwapo katika kauli hiyo kulikuwa na maneno ya kuhamasisha uasi, kuvuruga uchaguzi au “kukinikisha”. Mnyika amekanusha kuwepo kwa maneno hayo.Maswali hayo pia yamegusa uhusiano wa Lissu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Mnyika akikiri kuwa Lissu ni raia wa Tanzania na ana utii kwa Jamhuri hiyo. idha, Katuga amemuuliza kuhusu namna CHADEMA ilivyowaalika waandishi wa habari katika mkutano huo na iwapo chama kilitaka taarifa za mkutano huo kuwafikia wananchi.Haya ni baadhi ya maswali na majibu yaliyotokea kati ya Wakili wa Serikali Mkuu, Nasoro Katuga, na shahidi John Mnyika:Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kwa cheo chako wewe ndiye mtendaji mkuu?Mnyika: Sahihi.Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji Katiba ya CHADEMA ni moja ya nyenzo kuu ya utendaji kazi.Mnyika: Sahihi.Katuga: Ni public documents?Mnyika: Sahihi.Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Katibu Mkuu anapatikana vipi?Mnyika: Anapendekezwa na wanachama.Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa umesema hii Katiba ya CHADEMA unaifahamu, ni kweli CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi za Tanzania?Mnyika: Sahihi.Katuga: Na inasema CHADEMA inaamini katika uhuru na haki?Mnyika: Sahihi.Katuga: Ni sahihi kwamba dhumuni la CHADEMA ni kuhakikisha inashika dola kwa njia ya kizalendo?Mnyika: Sahihi.Katuga: Ni sahihi kwamba dhumuni kubwa ni kushika dola?Mnyika: Si sahihi.Katuga:Mnyika: Chama kina madhumuni ya kisiasa, kiuchumi na kijamii; kushika dola ni sehemu ya dhumuni.Katuga: Shahidi, labda uwaambie kiwango chako cha elimu, itanisaidia kuuliza aina gani ya maswali.Mnyika: Kidato cha sita.Katuga: Kwa kuwa elimu yako ni Kidato cha sita, nitakuwa sahihi nikisema huna uzoefu wa sheria?Mnyika: Sina uzoefu huo kwa sababu sijapita Law School.Katuga: Sasa hebu iambie Mahakama kama nilikusikia wewe ulisema wewe ni Afisa Masuhuli.Mnyika: Kweli.Katuga: Majukumu yako ni yapi?Mnyika: Kuidhinisha maombi ya matumizi ya fedha.Katuga: Ni kweli kwamba source za funds za CHADEMA zinatoka kwa wafadhili na marafiki?Mnyika: Kweli.Katuga: Kwa jukumu lako wewe ndiye mlipaji mishahara wafanyakazi wa CHADEMA?Mnyika: Naidhinisha, mimi siyo mlipaji.Katuga: Ni kweli kwamba hivi vyama vya siasa vina wafuasi wake?Mnyika: Kweli.Katuga: Kama Katibu Mkuu, kuna vyama vingapi vya siasa vyenye usajili?Mnyika: 19.Katuga: Ukiwa Mtendaji Mkuu wa CHADEMA, ni kweli kwamba hivi 19 ukiondoa CHADEMA vina wanachama wao na itikadi zao?Mnyika: Siwezi kuvisemea.Katuga: Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, ni kweli inatambua haki za wengine?Mnyika: Kweli.Katuga: Mwanachama wa CHADEMA ni lazima anaheshimu Katiba ya CHADEMA?Mnyika: Si lazima, anapaswa.Katuga: Na ni kweli asiyefuata anachukuliwa hatua?Mnyika: Sahihi.Katuga: Ulisema tarehe 3 Aprili ulikuwepo kwenye ule mkutano, waambie Waheshimiwa Majaji nani alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo?Mnyika: Hakukuwa na Mwenyekiti wa mkutano huo.Katuga: Shahidi, waambie Waheshimiwa Majaji uliwahi kuizungumzia hii kesi kwa kuwaita waandishi wa habari, kwamba mashahidi wa Jamhuri ni waongo?Mnyika: Nilisema Mwenyekiti hana hatia, ila siyo kuzungumzia hii kesi.Katuga: Kwa hiyo unaposema Mwenyekiti hana hatia au siyo mhaini, haya unayazungumzia kama shahidi au?Mnyika: Kwa mujibu wa maoni yangu na kwa ninavyomfahamu Mwenyekiti.Katuga: Ni sahihi kwamba wewe ni shahidi mwenye maslahi kwenye hii kesi?Mnyika: Hapana.Katuga: Kwanza unajua aina gani ya uhaini anayoshtakiwa nayo Tundu Lissu?Mnyika: Ninachojua mimi ni uhaini wa kuchapisha maneno ya kuitishia Serikali.Katuga: Sasa je, Lissu ana utii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?Mnyika: Ndiyo.Katuga: Je, yeye ni raia wa Tanzania?Mnyika: Ndiyo.Katuga: Je, huo mkutano wa tarehe 3 Aprili uliufuatilia?Mnyika: Sehemu kubwa nilifuatilia.Katuga: Kama nilikupata vizuri, ule mkutano wewe ndiye uliitisha, na ni mkutano wa ndani?Mnyika: Ndiyo.Katuga: Je, watia nia wote walifika?Mnyika: Sio wote.Katuga: Katika ushahidi wako kuna sehemu yoyote uliwaambia Waheshimiwa Majaji kwamba mbali na kumwalika Mwenyekiti, tulimwandikia risala ya kuzungumza?Mnyika: Hapana.Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ni nyinyi ndiyo mliomwandikia hotuba Mwenyekiti juu ya msimamo wa “No Reforms, No Elections”.Mnyika: Aliandika mwenyewe.Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji Katiba ya CHADEMA inasema inatambua demokrasia ya vyama vingi.Mnyika: Sahihi.Katuga: Uchaguzi Mkuu wa Tanzania upo kwa mujibu wa sheria?Mnyika: Upo kwa mujibu wa sheria.Katuga: Unajua kwamba Tanzania ina Katiba?Mnyika: Ndiyo.Katuga: Unajua kwamba Uchaguzi Mkuu upo kwa mujibu wa Katiba?Mnyika: Umewekwa kwa mujibu wa Katiba.Katuga: Sasa waambie Waheshimiwa Majaji, kama Uchaguzi Mkuu upo kikatiba, Mtanzania ana haki ya kushiriki?Mnyika: Ana haki ya kushiriki uchaguzi mkuu huru na wenye haki.Katuga: Ni haki kwa mwanachama wa CHADEMA kuzuia uchaguzi uliowekwa kikatiba?Mnyika: Ni haki kuzuia kwa njia za kidemokrasia.Katuga: Kama nilikusikia, mwanzilishi wa “No Reform” alikuwa nani?Mnyika: Freeman Mbowe.Katuga: Kwenye maneno ya “No Reforms, No Elections” kuna neno “tutahamasisha uasi”?Mnyika: Hakuna.Katuga: Kwenye hayo maneno kuna neno “tutakinukisha”?Mnyika: Hakuna.Katuga: Kuna sehemu kuna maneno yanayosema tunaenda kuuvuruga uchaguzi?Mnyika: Hivi shahidi, nimekusikia ukizungumza mengi ukiyarejea yale aliyozungumza Mwenyekiti, uliyasikia au?Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema umeithibitishia Mahakama hii kwamba haya maneno uliyoyasikia ni mshtakiwa ameyatoa?Mnyika: Nimeyasikia.Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema kwamba uliwaita waandishi wa habari kurusha kile mlichozungumza?Mnyika: Kurusha kwa uhuru wao.Katuga: Mliwapa tahadhari kwamba wachapishe kile tu wanachoona kinafaa?Mnyika: Hatukuwapa, tunaheshimu uhuru wa habari.Katuga: Mliwapa hotuba ile ya Mwenyekiti kwamba atazungumza hivi?Mnyika: Nilishalijibu.Katuga: Mtu anayefanya live streaming, nitakuwa sahihi kwa mujibu wa sheria maana yake ni kusambaza taarifa?Mnyika: Sio lazima.Katuga: Sasa kwa kuwa umeiambia Mahakama hii kwamba nia ya kuwaita waandishi wa habari ni kuchukua habari kwa uhuru wao…Mnyika: Tuliwaita lakini hatukuwalazimisha.Katuga: Nyinyi mnataka taarifa ziwafikie umma, hapa Mahakamani tuna ushahidi kwamba Jambo TV ndiyo chombo pekee kinachotangaza habari za CHADEMA bila woga.Mnyika: Hilo sifahamu.Katuga: Kutolifahamu na kulifahamu ni jambo lingine. Hili ni la kweli au siyo, kulizungumzia kweli?Mnyika: Sijui.Kesi imeahirishwa mpaka kesho saa nne asubuhi ambapo Mnyika anatarajiwa kumaliza sehemu ya ushahidi wake