Wahamiaji 43 wakiwemo watoto wachanga watatu walifariki baada ya mashua yao kupinduka katika pwani ya Tarfaya kusini mwa Morocco, shirika la Uhispania la Caminando Fronteras lilisema Jumatatu.
Watu kumi waliokolewa kutokana na ajali hiyo ya mashua, msemaji wa shirika hilo aliambia AFP.
Walionusurika walikuwa wamepiga simu wakiomba uokoaji asubuhi ya Jumapili, na waliweza kudumisha mawasiliano kwa saa mbili.
“Ilichukua saa kadhaa kwa mamlaka ya Morocco kutambua mashua ilipokuwa na kuwaokoa” Caminando Fronteras alisema ambaye hushughulika na kufuatilia data kutoka kwa boti zilizo taabani.
Ni miili miwili pekee ndiyo iliyopatikana kati ya miili 43, lilisema shirika hilo, ambalo lilizingatia ushuhuda wa walionusurika na familia za wahasiriwa.
Wahamiaji hao walikuwa wakielekea Visiwa vya Kanari vya Uhispania, kilomita 100 (maili 62) kutoka Tarfaya.
Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ni njia muhimu kwa wahamiaji wanaotoka barani Afrika kuelekea Ulaya.
Kulingana na Caminando Fronteras, zaidi ya wahamiaji 4,000 waliuawa au kutoweka mwaka jana wakijaribu kuelekea Uhispania, mara mbili zaidi ya wale wa mwaka wa 2020.
Miili ya wengi haikupatikana.
Kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Uhispania, zaidi ya wahamiaji 373,000 waliwasili nchini kwa njia ya bahari mnamo 2021.