Mrema kuzikwa Agosti 25 kijijini kwao

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema unatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi Agosti 25 katika kijiji cha Kiraracha mkoani Kilimanjaro

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtoto wa Mrema, Michael Mrema Maziko hayo yatatanguliwa na ibada ya mazishi siku ya Jumatano itakayofanyika katika kanisa Katoliki Parokia ya Salasala kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro. 

Mrema ambaye ni mwanasiasa mkongwe  aliyefariki dunia jana Jumapili Agosti 21,2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

https://mwanzotv.com/2022/08/22/augustine-lyatonga-mrema-mwanasiasa-aliyetamba-kwenye-ulingo-wa-siasa-na-kuacha-gumzo-kila-mahali/