Search
Close this search box.
Africa

Msimamizi wa gereza ajiua kwa kujipiga risasi

8

Msimamizi wa gereza anayesimamia katika gereza la Kodiaga Maximum kaunti ya Kisumu amejiua akiwa kazini katika kile kinachoaminika kuwa ugomvi wa kinyumbani.

Tukio hilo limetokea usiku wa Machi 23, ambapo Afisa huyo ambaye jina lake halikutajwa inaelezwa kuwa  alijipiga risasi kwa kutumia bunduki yake aina ya G3 kwenye lango la gereza alilokuwa akilisimamia na kufariki dunia papo hapo.

Kulingana na ripoti ya polisi, afisa huyo alikuwa amelewa.Inaarifiwa kuwa mkewe alifika langoni na kumwomba pesa za chakula lakini afisa huyo alikataa akisema hana.

Polisi wamesema muda mfupi baadaye, alisikika akimwambia mke wake awatunze watoto wao bila kumsahau na mama yake kwa kuwa muda sio mrefu anaenda kufa. 

Makachero kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na askari wa kituo cha polisi cha Maseno walitembelea eneo la tukio na jalada la uchunguzi limefunguliwa.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Jaramogi Oginga Odinga

Related Tag:

Comments are closed

Related Posts