Mtoto ajeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea leo Ukraine

Takriban watu sita wamejeruhiwa, akiwemo mtoto, katika mlipuko uliotokea leo katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine mlipuko huo uliharibu jengo la serikali, na kuzidi kuleta hofu kwa raia.

“Urusi inaendesha vita kinyume na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Inaua raia, inaharibu miundombinu ya raia. Lengo kuu la Urusi ni miji mikubwa ambayo sasa inarushwa na makombora yake,” 

Video tofauti zilizotumwa na Mkuu wa Wafanyakazi wa Ulinzi wa mji wa Kharkiv, bwana  Kostiantyn Nemichev,, zilionyesha matokeo ya mlipuko huo unaodaiwa, ikiwa ni pamoja na ndani ya jengo ambalo lilikuwa limeharibiwa na kuwa kifusi.

Hali bado ni tete nchini Ukraine kwani hadi sasa raia wa Ukraine na wasiokuwa raia wa nchi hiyo maisha yao yako hatarini zaidi kutokana na vita inayoendelea licha ya kutolewa matamko ya kusitisha vita hivyo.

Hivi sasa mataifa mengi ulimwenguni yenye raia wake nchini Ukraine yanahangaika namna ya kuwaondoa raia wake nchini humo hadi pale hali ya utulivu itakaporejea.

Inakadiriwa kuwa takriban wanajeshi 70 wa Ukraine wameuawa katika shambulio la mizinga la Urusi.