Mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Magufuli

Hayati Dk. John Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania

Leo ni kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo ibada maalum imefanyika kwa ajili ya kumuombea.

 Hayati Magufuli alifariki Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam kutokana na tatizo la moyo.

Kifo cha Magufuli kimeiingiza Tanzania kwenye historia ya nchi chache duniani ambazo viongozi wake walifariki wakiwa madarakani.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 62, huku akiacha mke, watoto na wajukuu.

Anakumbukwa kwa mengi ikiwemo aina yake ya uongozi ambao wengi wameutazama kwa namna tofauti ikiwemo kuutafsiri uongozi wake kama wa kimabavu.

Pia Hayati Magufuli anakumbukwa kwa namna ambavyo alivyopambana kwa namna tofauti juu ya ugonjwa wa corona, aliamini sana dawa za asili kuliko chanjo zilizoelekezwa na Shirika la Afya duniani, WHO.

Leo Watanzania wanakumbuka mwaka mmoja tangu kufariki kwake lakini je nini kilitokea ?

Tazama safari yake hapa

https://youtu.be/HrZacdSFrb4