Search
Close this search box.
Africa
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP, Ally Makame.

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamshikiria mwalimu wa mafundisho ya dini katika Kanisa la Katoliki Mpanda Mjini, Joseph John (27) akituhumiwa kuwalawiti watoto wanne.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ACP, Ally Makame amesema mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo katika maeneo tofauti mkoani humo.

Amesema mtuhumiwa  alikamatwa Februari 03, 2022 akiwalaghai watoto hao wamsindikize kwenda kufanya shughuli za biashara sehemu tofauti, na alikuwa akiwabeba kwenye pikipiki yake

“Alikuwa anawabeba kwenye pikipiki yake baada ya kumaliza vipindi vyao vya masomo ya kidini kisha kuwafanyia ukatili huo,Baada ya kumkamata tulimhoji akakiri kufanya hivyo, lakini baadhi ya watoto tuliowahoji wamekubali kufanyiwa,” amesema Makame.

Kamanda Makame amesema upelelezi wa shauri lake umekamilika na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Kutokana na hali hiyo ametoa rai kwa viongozi wa taasisi za kidini kutojihusisha na uovu kwa kigezo cha kutumia imani zao.

“Wazazi walimuamini kuwa yeye ni mwalimu nisisitize tabia hiyo ikome ni ukiukwaji wa sheria na inaathari kubwa kwa watoto,” amesema.

Comments are closed