Search
Close this search box.
Africa

Polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wamemkamata mwanafunzi wa udaktari anayedaiwa kughushi utekaji nyara wake mwenyewe ili kudai kikombozi kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mujibu wa BBC Edwin Kamau (23), anatuhumiwa “kutoweka” siku ya Jumapili na kumpigia simu mama yake siku chache baadaye kuomba fidia ya Ksh 70,000 (Tsh 1,380,000).

Awamu ya kwanza ya fidia hiyo ililipwa siku ya Jumatano, lakini polisi wanasema mwanafunzi huyo alienda kulewa nje kidogo ya jiji na mwanamke ambaye aliongeza kinywaji chake na kuiba pesa hizo.

Siku ya Alhamisi, alidai na kulipwa awamu ya pili ya fidia hiyo lakini akamatwa muda mfupi baadaye na pesa hizo zikapatikana zikiwa zimewekwa kwenye viatu vyake.

Polisi wanasema mwanafunzi huyo alikiri kufuja pesa zilizokuwa zikilipwa karo ya muhula uliopita na kughushi utekaji nyara wake ili kutafuta pesa. Mshukiwa anasubiri kufikishwa mahakamani.

Comments are closed