Mwanafunzi nchini Kenya afanya mtihani wa Taifa baada ya kujifungua

a

Mtahiniwa mmoja wa Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane nchini (KCPE) katika kaunti ya Kisii nchini Kenya anafanya mtihani huo katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii (KTRH) baada ya kujifungua siku moja kabla ya mtihani huo.

Katibu Mkuu wa Elimu, Julius Jwan ambaye alizungumza baada ya kushuhudia kufunguliwa na kusambazwa kwa mtihani huo unaoanza leo nchini humo, kutoka kaunti ndogo ya Kisii ya Kati hadi vituo vya mitihani.

Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) watahiniwa 1,225,507 wanafanya mtihani huo katika vituo 28,316 ikilinganishwa na mwaka 2020 ambapo watahiniwa walikuwa 1,191,752 katika vituo 28,467.

Kwa mujibu wa agizo la Wizara ya Elimu, ni manaibu makamishna wa Kaunti (DCC) na Kamishna Wasaidizi wa Kaunti (ACC) ambao wanaruhusiwa kufungua na kufunga mashehena ya mitihani katika Kaunti Ndogo zao na Mitihani yote inasafirishwa kutumia magari ya serikali na kwa ulinzi wa angalau afisa mmoja wa polisi.

Mameneja wa vituo watashirikiana na maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa hakuna kataratasi au maswali yanafikia watahiniwa kabla ya muda rasmi wa karatasi hilo kufanywa.

Maafisa mbalimbali wa serikali wakiwemo mawaziri na makatibu wamejitokeza kwa uangalizi wa mwanzo wa zoezi hilo hii leo wakiongozwa waziri wa Elimu George Magoha na mwenzake wa Usalama Fred Matiang’i.

Mtihani ya kitaifa ya darasa la nane (KCPE) imeanza rasmi  hii leo nchini Kenya ikitarajiwa kukamilika Machi 9,2022.