Search
Close this search box.
Africa

Mwanafunzi wa darasa la tatu auwawa Tanga

12

Jeshi la polisi mkoani Tanga linamshilikia mtoto wa miaka (9) mkazi wa mji mpya Hale ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi kichangani darasa la tatu iliopo wilayani Korogwe mkoani Tanga Kwa kosa la mauwaji ya Ally khalifa Bakari (9) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kichangani mkazi wa Msalo Hale.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Safia Jongo, amesema mauwaji hayo yametokea leo majira ya saa nane mchana mara baada ya wanafunzi hao kutoka msikitini.

Amesema tayari maafisa wa polisi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi wilayani Korogwe wamefika katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jongo amesema mwili wa marehemu umekutwa na majeraha mengi sehemu mbalimbali za mwili wake hivyo uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini kama tukio hilo limefanywa na mwanafunzi huyo pekee.

Comments are closed

Related Posts