Mwanamke afanya ngono na mtoto wa darasa la tatu nchini Tanzania

Jeshi la Polisi mkoani Iringa nchini Tanzania, linamshikilia mwanamke mmoja nchini humo mwenye umri wa miaka 56 kwa tuhuma za kumdhalilisha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 na kumsababishia maumivu pamoja na majeraha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, amesema tukio hilo lilitokea Mei 8, 2022  Kijiji cha Lumuli kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Amesema kuwa mtuhumiwa, Desderia Mbelwa alimkamata kwa nguvu mtoto huyo anayesoma darasa la tatu alipokuwa anatoka shule na kumvutia kichakani.

Baada ya kumvutia kichakani alimtishia asiseme na kufanya nae ngono kitendo kilichomsababishia mtoto huyo maumivu makali na majeraha sehemu zake za siri.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, Desderia amekiri kutenda kosa hilo bila kutaja sababu za yeye kufanya hivyo na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.