Mwanamke aliyekosa kushiriki kitendo cha ndoa kwa miaka 19 ampa mumewe talaka

Mwanamke aliyekuwa katika ndoa kwa miaka 19 bila kushirki kitendo cha ndoa amempa mumewe talaka.

Rebecca Magaba alimpa mumewe Zablon Maselenge talaka baada ya kuvumilia miaka 19 bila kitendo cha ndoa.

Rebecca Magaba

Rebecca anasema alikutana na mumewe mapema mwaka 2000 walipochumbiana na kisha kufunga ndoa.Ila mumewe Zablon hakuwahi kufichua kuwa alikuwa na ugonjwa wa Cryptorchidism. Cryptorchidism ni tatizo la kiafya ambapo korodani zinasalia tumboni badala ya kushuka.

Zablon alifichua hali yake wiki kadhaa baada ya kufunga ndoa na Rebecca akihofia iwapo angemweleza mapema, Rebecca hangekubali kuwa katika ndoa nae.

Rebecca Magaba alisalia katika ndoa kwa miaka 19 bila kushiriki kitendo cha ndoa na mumewe Zablon Maselege, ambaye kwa tatizo lake hangeweza kumtimizia mkewe majitaji yake ya ndoa.

Baada ya miaka kadha ya kuwa katika ndoa ambayo hatoshelezwi, Rebecca alitafuta usaidizi kutoka kwa makasisi waliofanya mkutano na mumewe. Maselenge alifichua siri yake baada ya mkutano wake  na makasisi na kusema kuwa kutokana na hali yake hajawahi kushiriki kitendo cha ndoa maishani mwake na pengine hatawahi kushiriki kitendo hicho.

Rebecca anasema alivumilia kukaa kwa ndoa hiyo kwasababu alimpenda mumewe, ila Maselege alianza kumshuku mkewe kuwa alikuwa na wapenzi wa nje, na akawa akimpiga mara kwa mara akidai kuwa Rebecca hana uvumilivu nae.

Wedding Rings symbolizing the divorce between two people

Jaji Mwinyiheri Kondo aliamua kuwapa talaka wawili hao baada ya kuamua kuwa Rebecca na mumewe walikuwa hawajatimiza masharti ya kuwa katika ndoa inayotambuliwa na sheria. Mahakama iliamua kuwa mali waliopata pamoja katika ndoa yao ya miaka 19 igawanywe sawa kati yao.