Search
Close this search box.
Africa

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Rombo na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Boma iliyopo Tarafa ya Mkuu Wilayani humo, Turo Hiza  amekutwa ameuawa na kisha mwili wake kutelekezwa barabarani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ,Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Hamis Maiga amesema mwili wa Mwalimu huyo umekutwa usiku wa kuamkia leo ,Mei 26, 2022 eneo la Mrere Mashati karibu na Shule ya Sekondari Shauritanga iliyopo wilayani humo.

“Tukio hili limetokea leo majira ya saa 10 alfajiri eneo la Mrere Mashati,karibu na shule ya Sekondari Shauritanga ambapo mwili wa mwalimu Hiza umekutwa barabarani huku damu zikiwa zinachuruzika kwenye lami,” amesema Maiga.

Amesema chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana na kwamba mwili wake umekutwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Hata hivyo baada ya mwalimu huyo kuuawa wauaji hao waliondoka na pikipiki yake ambayo alikuwa  akiitumia kama usafiri wa kwenda kazini.

Mwili wa mwalimu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma wilayani humo.

Comments are closed