Ndolezi atia nia kuwania ubunge Kigoma Kusini

Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu-Bunge, Sera, Vijana , Kazi na Ajira ACT Wazalendo Mhandisi Ndolezi Petro ametangaza nia rasmi ya Kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini. 

Ameeleza pia msukumo wake wa  kutia nia ya kugombea nafasi hiyo umetokana na changamoto wananchi wanazopitia. Amesema Jimbo la Kigoma Kusini linakumbwa na changamoto za Miundombinu ya Barabara, Changamoto za ukosefu wa pembejeo za kilimo, migogoro ya ardhi, huduma za afya kwenye vituo vya Afya na amesema sera na mipango itaelezwa vizuri wakati wa kampeni akipata ridhaa ya kugombea Jimbo la Kigoma Kusini.

Ikumbukwe kuwa Chama cha ACT Wazalendo kilifungua milango kwa watiania nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani rasmi kupitia Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu, Ado Sahibu tarehe 15 Januari,2025.

Tangu pazia lifunguliwe kwa upande wa Urais hadi sasa waliotia nia ni wawili. Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyetangaza nia ni Ndugu, Dorothy Semu ambaye kwa Sasa ni Kiongozi wa Chama na Kwa upande Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar ni Ndugu, Othman Masoud Othman Sharif ambaye Kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.