Nigeria kufunga mipaka yake siku ya uchaguzi

Nigeria imeamuru kufungwa kwa mipaka yake yote ya ardhi wakati wa uchaguzi utakaofanyika Jumamosi wenye ushindani mkali.

Maagizo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa “uchaguzi huo ni huru, wa haki na hauna dosari”, Idara ya Uhamiaji ya Nigeria ilisema.

Maafisa wa mpaka wameambiwa kuhakikisha utekelezwaji mkali wa agizo hilo.

Uchaguzi wa rais na bunge unaripotiwa kuwa na upinzani mkali zaidi tangu utawala wa kijeshi kumalizika mwaka 1999.

Idara ya uhamiaji ilisema imekamata kadi za wapiga kura 6,000 na hati nyingine za utambulisho wa Nigeria kutoka kwa wahamiaji haramu katika kipindi cha maandalizi ya uchaguzi.

Rais Muhammadu Buhari mapema Alhamisi alivitaka vyombo vya usalama kuwa “imara na ujasiri” katika kipindi cha uchaguzi, na kuonya dhidi ya ghasia baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.