Search
Close this search box.
Africa

Jeshi la Polisi mkoani Katavi nchini Tanzania, linamshikilia Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Dickson Mwenda (37), kwa tuhuma za kunajisi mtoto wa miaka 15 ndani ya gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame amewaambia wanahabari kuwa, tukio hilo lilitokea Agosti 13, 2022, majira ya saa moja na nusu jioni katika Kijiji na Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele.

ACP Makame amesema, mama mzazi wa binti huyo, alikuwa pamoja Bar na mtuhumiwa na watu wengine wakipata vinywaji, lakini ulifika wakati alimkabidhi mtuhumiwa mtoto huyo akiwa na mdogo wake, kwa lengo la kuwapeleka nyumbani.

Hata hivyo akiwa njiani na watoto hao katika gari yake yenye namba za usajili T. 927 DMC, inadaiwa aliegesha gari pembeni ya barabara, kisha akatekeleza unyama huo.

Comments are closed