Jeshi la Polisi limezingira jengo la makao makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema muda mchache kabla ya kufanyika mkutano wa Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, ambaye alitangaza kuzungumza na wanahabari leo Januari 27,2025 mapema asubuhi
Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Jeshi la Polisi au Chadema kuhusu nini chanzo cha uwepo wa askari hao ambao wamezuia waandishi wa habari waliofika kwa ajili ya mkutano uliopaswa kufanyika saa tano asubuhi kamili.
Inadaiwa uwepo wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati (M300) huenda ikawa sababu ya mkutano huo cha Chadema kuzuiwa.
Tanzania inapokea marais wapatao 24 kutoka nchi mbalimbali ambao watahudhuria Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika utakaofanyika leo Januari 27 na 28 mwaka huu kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.