Rais Samia: Kila la kheri Wakenya 

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amewatumia Wakenya salamu za heri wakati wakipiga kura katika uchaguzi mkuu unaofanyia leo August 9,2022

Rais Samia ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiwataka Wakenya kudumisha amani, umoja na mshikamano.

“Nawatakia majirani zetu wa Kenya uchaguzi mwema. Ninaomba kwamba Mungu awe pamoja nanyi mnapotimiza haki yenu ya kikatiba ya kupata viongozi mnaowataka,” alisema kwenye ukurasa wa tweeter.

Amewataka Wakenya “kudumisha amani, umoja na mshikamano” na kuongeza “kila la kheri”.

Majirani wa Afrika Mashariki wa Kenya wanatarajia uchaguzi mzuri ili kuepusha kuvurugika kwa uchumi wa kanda – huku Kenya ikiwa kiungo kikuu cha Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ghasia zilizofuata baada ya uchaguzi wa 2007 zilitatiza mtiririko wa bidhaa katika eneo hilo.

Takribani Raia milioni 22 wa Kenya leo wanatarajiwa kupiga kura kuchagua viongozi wa Serikali Kuu na serikali za mitaa. Kwa Wananchi wa Kenya  watapiga kura sita ambapo watamchagua Rais, Gavana wa Kaunti, Seneta, Mbunge, Mwakilishi wa wanawake bungeni na Diwani

Uchaguzi Mkuu nchini Kenya hufanyika kila baada ya miaka mitano. Katika miaka ya hivi karibuni Kenya  imekuwa ikikumbwa na mizozo wakati wa uchaguzi, kwa mfano shuhudio la uchaguzi wa urais mnamo mwaka 2007.