Rais wa Hungary, Katalin Novak anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.Kiongozi huyo anawasili nchini kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo takuwa nchini kwa siku nne kuanzia leo hadi Julai 20 mwaka huu.
Katalin ni mwanasiasa maarufu nchini Hungary ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo katika uchaguzi wa mwaka jana.
Katalin ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini humo na pia ndiye Rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Hungary. Alichaguliwa akiwa na umri wa miaka 44. Kabla ya kushika wadhifa huo, mwanamama huyo alikuwa Waziri anayehusika na Sera za Familia.