Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Rais wa Tanzania atajwa kuwa ni miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi - Mwanzo TV

Rais wa Tanzania atajwa kuwa ni miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi kwa mwaka 2022 na jarida la TIME katika kitengo cha viongozi wa kisiasa.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Rais Samia amekuwa chachu na ameleta mabadiliko makubwa kwa Tanzania tangu aingie madarakani Machi 2021.

“Mlango umefunguliwa kwa mazungumzo kati ya wapinzani wa kisiasa, hatua zimechukuliwa, ili kujenga upya imani katika mfumo wa kidemokrasia, juhudi zimefanywa kuongeza uhuru wa vyombo vya habari, wanawake na wasichana wana mfano mpya wa kuigwa,” linaandika TIME.

“Mnamo Septemba 2021, miezi michache tu baada ya urais wake, Rais Samia alitoa hotuba ya kihistoria kama kiongozi wa tano pekee wa Kiafrika aliyewahi kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa .Alisimama mahali ambapo mmoja alisimama miaka 15  kabla ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa kidemokrasia barani Afrika”.

Orodha hiyo imekuja wakati ambapo Rais Samia pia akipangwa kupokea tuzo ya Africa Road Buildersā€“Babacar Ndiaye Trophy 2022 kwa kutambua dhamira yake katika maendeleo ya miundombinu ya usafiri.

Tuzo hyo ambayo ilichukuliwa na Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, mwaka jana, itakabidhiwa kwa Rais Samia katika mkutano wa mwisho wa Wajenzi wa Barabara Afrika, ambao umepangwa kufanyika pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), mkutano wa kila mwaka huko Accra, Ghana.

Mbali na kiongozi huyo wa Tanzania, Orodha ya TIME 100 yenye ushawishi zaidi inajumuisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin.

Wengine ni Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, mwanatenisi Rafael Nadal, Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook na mogul wa vyombo vya habari Oprah Winfrey.