Ruto ahitimisha ziara yake nchini Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania, ambapo katika ziara hiyo Kenya na Tanzania zimekubaliana kumaliza vikwazo vya biashara visivyo vya kikodi, kukuza ushirikiano katika mawasiliano, utalii na kudhibiti ugaidi na usafirishaji wa binadamu.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Rais Ruto ameagwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax.

Kwa ziara hiyo, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kwa Rais Ruto kufanya ziara ya kikazi, na nchi ya tano kutembelea dunia tangu aapishwe Septemba 13 mwaka huu, ikitanguliwa na Uingereza, Marekani, Ethiopia na Uganda.