Search
Close this search box.
Sports

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini humo imekuwa kwa kiasi kikubwa na imeanza kuleta tija kwa maisha ya Watanzania kutokana na miongozo thabiti inayotolewa na Serikali

“Kwenye Sanaa tumeona namna ambavyo nchi hii imeweza kutangazwa vizuri na wasanii wengi kutoka ndani ya nchi, haya yote ni matokeo ya uratibu unaofanywa na Wizara, kwenye michezo tumeona namna ambavyo leo hii Tanzania inavyopata heshima kwa kuwa na timu za michezo mbalimbali zikifanya vizuri ndani na nje ya nchi.”

Majaliwa amesema Sekta ya  Utamaduni, Sanaa na Michezo imeonesha kuwa na uwezo wa kutoa ajira kwa vijana wengi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla huku akitanabaisha kuwa sasa kwenye michezo kuna vijana wa Kitanzania wanaocheza michezo ya kulipwa katika nchi mbalimbali.

Aidha amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili kuwawezesha Maafisa Utamaduni na Michezo kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara hiyo kuhakikisha inaboresha uratibu na usimamizi wa mafunzo ya wataalamu wa michezo nchini ili kuongeza idadi ya wataalam hao hususani katika mpira wa miguu

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, Omari Mchengerwa amesema Sekta ya michezo nchini humo imeendelea kuimarika na imechangia zaidi ya shilingi bilioni 1.7 katika pato la Taifa na Wizara imeendelea kujipanga ili kuhakikisha mchango wa sekta hiyo inafikisha shilingi  bilioni 3 kwa mwaka wa fedha 2022/20

Comments are closed