Serikali ya Tanzania yaondoa tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta

Serikali ya Tanzania imetangaza kuondoa tozo ya shilingi 100 kwa lita ya mafuta ya Dizeli, mafuta ya Taa na Petroli zinazopaswa kulipwa na watumiaji wa mafuta kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia 2 Machi 2022.

Hatua hii ni  kutokana na kupanda kwa bidhaa hizo katika soko la dunia iliyosababishwa na vita vya Urusi na Ukraine.

Uamuazi huo uliotolewa utaipunguzia serikali  mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa mwezi yaliyokuwa yanakusanywa kila mwezi.

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Nishati nchini humo imeeleza kuwa serikali imeona umuhimu wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya athari za mabadiiko ya bei za mafuta ulimwenguni.

Uamuzi huo umeenda sambamba na maelekezo ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa baada ya kikao na Wizara ya Nishati nchini humo pamoja na taasisi zinazohusika na masuala ya nishati  mnamo oktoba 5 2021 ambacho kiliazimia kupunguza tozo mbalimbali zenye thamani ya shilingi bilioni  102 kwa watumiaji wa mafuta nchini.