Search
Close this search box.
Africa

Sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar zimepangwa kufanyika Aprili 26 jijini Dodoma, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu nchini Tanzania, George Simbachawene amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika tofauti na ilivyozoeleka.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini humo kwa kufanyika uzinduzi wa andiko yaani kitabu cha historia ya Muungano pamoja na kongamano.

Alisema pia kamati ya maandalizi kwa kushirikiana na Tamisemi imeandaa mashindano ya insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchi nzima.

Simbachawene amesema taasisi za serikali na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitaadhimisha kwa kufanya shughuli za kijamii katika maeneo yao ya karibu au vikosi na kambi kama vile kufanya usafi, kupanda miti na kutoa huduma za afya.

Pia kutakuwa na maonesho yatayofanyika Zanzibar kuanzia leo April 21 hadi Mei 6, mwaka huu yakihusisha taasisi za Muungano.

Itakumbukwa sherehe za Muungano zimezoeleka kufanyika katika maeneo ya wazi ambayo ni viwanja vikubwa huku yakipambwa na maonyesho mbalimbali kama gwaride, ngoma za asili na maonyesho mengineyo.

Comments are closed