Mji mkuu wa Libya Tripoli hivi majuzi ulifanya tukio lisilo la kawaida lakini la kuvutia—shindano lake la kwanza la urembo kwa kuku—lililovutia wageni na washiriki kutoka kote nchini.
Waandaalizi wa hafla hiyo walisema kuwa hafla hiyo ilifanyika sio tu kwa ajili ya kuhamasisha ufugaji wa kuku bali pia kutoa fursa kwa vijana wafahamu kuhusu ufugaji wa kuku na faida yake ili wasijihusishe na migogoro inayoendelea nchini.
“Tunashuhudia mkusanyiko wa wafugaji wa kuku kwa madhumuni ya mapambo. Hii ni taaluma kubwa ambayo imewaondoa vijana kutoka kwa maovu na vita.
“Natumai viongozi watawaunga mkono vijana katika nyanja hii,” Khaled Diab alisema.
Diab aliongeza kuwa ndege walioshiriki katika hafla hiyo walistahili kushiriki katika mashindano ya kimataifa pia.
Ndege hao waliwekwa katika mizani ya urembo kwa kuzingatia rangi ya manyoya yao na ukubwa umbo lao.
Taher Belkassem, ambaye alitembelea shindano hilo alisema kuwa hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuona kitu kama hiki.
Nilikuwa nikisikia kuku wa kawaida tu hapo awali, hii ni mara yangu ya kwanza kuona aina tofauti ya kuku.
Huu ni mpango mzuri na ninawashukuru waandaalizi kwa juhudi zao,” alisema.
Mohannad Jaydeh, ambaye kuku wake aina ya Brahma ilishinda shindano hilo kwa asilimia kubwa zaidi ya 93.8, alisema, “Kuku huyu anajulikana kwa ukubwa wake na miguu yake ya njano.
Pia anajulikana kwa anavyokunja uso wake, ulaini na kung’aa kwa manyoya yake.”