Simba kurejea Tanzania kinyonge

Klabu ya SIMBA inatarajiwa kurejea nchini leo mchana majira ya saa saba ikitokea Morocco baada ya kumalizika kwa michezo yao miwili ya Kombe la Shirikisho.

Awali Simba ilikuwa nchini Niger, kucheza na USGN na kutoka sare ya 1-1 kisha ikaenda Morocco kuvaana na RS Berkane ambao waliwaadhibu Simba kwa mabao 2-0. 

Taarifa iliyotolewa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally, imesema, Simba inarejea nchini kupitia Dubai.