Uongozi wa klabu ya Simba nchini Tanzania imesema ndugu Mugarami Said Mohamed maarufu kama Shilton hakuwa muajirwa wa klabu hiyo
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 15 na klabu ya Simba ni kwamba klabu hiyo ilimuomba na kukubaliana na ndugu Muharami kuwanoa Makipa wa Simba kwa muda wa mwezi mmoja wakati huo klabu ikiendelea kutafuta kocha wa Magolikipa.
Klabu hiyo imesema haihusiki na tuhuma zinazomkabili kocha huyo.
Uongozi wa Simba umewaomba mashabiki wake kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba kocha huyo.
Muharami anadaiwa kukutwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi.