Somalia mwanachama kamili Jumuiya ya Afrika Mashariki

Somalia sasa  imekuwa mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya kukamilisha hatua zote zilizohitajika ili kuidhinishwa kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Kupitia ukurasa wa X, zamani Twitter ya EAC leo Jumatatu taarifa imeeleza kwamba Somalia imepata uanachama kamili “baada ya kuwasilisha Hati yake ya Kuidhinishwa kwa Katibu Mkuu” wa jumuiya hiyo.

Somalia inakuwa mwanachama wa nane wa EAC baada ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.

Chombo cha uidhinishaji ni hati rasmi iliyotolewa na nchi, ambayo inakubali kufungwa na mkataba.

Novemba mwaka jana, wakuu wa nchi nyingine wanachama wa EAC walikubali kujumuishwa kwa Somalia katika umoja huo.

Hatua hiyo inanuiwa kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini humo, ambao bado unaendelea kuimarika kutokana na miongo mitatu ya vita