Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan siku ya Jumapili aliondoa hali ya hatari iliyowekwa tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana, baraza kuu linalotawala lilisema.
Sudan imekuwa ikikabiliwa na machafuko yanayozidi kuongezeka tangu Burhan aongoze mapinduzi ya Oktoba 25, na hivyo kuhitimisha mpito dhaifu baada ya kuondolewa kwa rais Omar al-Bashir mwaka 2019.
Burhan ‘alitoa amri ya kuondoa hali ya hatari nchini kote’, baraza hilo lilisema katika taarifa.
Agizo hilo lilitolewa “ili kuweka nafasi kwa mazungumzo ambayo yatafikia utulivu kwa kipindi cha mpito,’ iliongeza.
Uamuzi wa Jumapili ulikuja baada ya mkutano na maafisa wakuu wa kijeshi kupendekeza hali ya hatari iondolewe na watu waliozuiliwa chini ya sheria ya dharura waachiliwe.
Pia imekuja baada ya mwito wa hivi punde wa mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Volker Perthes wa kuondoa hali ya hatari, kufuatia mauaji ya waandamanaji wawili wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi siku ya Jumamosi.
Sudan imekumbwa na maandamano makubwa tangu mapinduzi hayo, ambayo yamekabiliwa na msako mkali ambao umesababisha karibu watu 100 kuuawa na mamia kujeruhiwa, kulingana na matabibu wanaounga mkono demokrasia.
Mamia ya wanaharakati pia wamesakwa kwenye chini ya sheria za dharura.
Siku ya Jumapili, maafisa wa kijeshi pia walipendekeza kuruhusu kitengo cha televisheni cha moja kwa moja cha mtandao wa Al Jazeera wenye makao yake Qatar kuanza tena operesheni nchini Sudan, baada ya mamlaka kukipiga marufuku mwezi Januari kwa kuangazia maandamano.
Unyakuzi huo wa kijeshi ulizua shutuma nyingi za kimataifa na adhabu , ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa misaada muhimu kutoka kwa serikali za Magharibi hadi pale utawala wa kiraia utakaporejeshwa.