Polisi watanda Dar es Salaam, Viongozi wa upinzani wakamatwa
Polisi wa kupambana na ghasia wamekusanyika katika maeneo kadhaa katika jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo, kuelekea maandamano ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).