Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu kuanza kuunguruma Mahakama Kuu ya Tanzania Septemba 12
Ikumbukwe Agosti 18, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilibainisha kuwa kesi hiyo inakwenda Mahakama Kuu baada ya hatua za Kisheria kukamilika.
Ikumbukwe Agosti 18, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilibainisha kuwa kesi hiyo inakwenda Mahakama Kuu baada ya hatua za Kisheria kukamilika.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema kwamba kazi ya chama hicho kwa sasa ni kuisaka dola kwani mchakato wa kura za maoni zilishapita hivyo hakuna sababu ya kuwa na mgawanyiko tena.
“Najua kulikuwepo na maneno au vijineno eti utaratibu umekiukwa na mimi nililaumiwa kwa jinsi nilivyosema pale kwenye mkutano mkuu, lakini nasema waliokuwa wanasema hayo ama hawafahamu utaratibu wa chama chetu na kama wanafahamu labda wamesahau au wanajifanya hamnazo,” alisema Kikwete.
Moja ya madai makuu ya CHADEMA ni mageuzi ya kisheria na mchakato wa uchaguzi, ambapo wanataka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) irekebishe taratibu za uteuzi na usajili wa wagombea ili vyama vyote viwe na nafasi sawa, bila upendeleo kwa chama tawala.
Kwa mujibu wa INEC, jumla ya vyama 18 vilivyosajiliwa vitashiriki uchaguzi huu, na wagombea 17 wa urais watashiriki kinyang’anyiro
Ahadi hiyo imetolewa jana katika mazungumzo yake na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, yaliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Katika taarifa yake kwa umma, chama hicho kimeeleza kuwa hatua ya Msajili haina mashiko ya kisheria kwa kuwa mchakato wa uchaguzi tayari umeshaanza, huku Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiwagawia wagombea fomu za kugombea urais. Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, Msajili hana mamlaka ya kuingilia hatua hiyo, zaidi ya kushughulikia malalamiko kwa njia ya pingamizi.
Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) imeitolea wito Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha inalinda, inaheshimu na inatekeleza kwa dhati viwango vya haki za binadamu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025.
Kipindi cha uongozi wake kama Spika kiligubikwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani waliomtuhumu kwa upendeleo, kufungia wabunge waliokuwa wakikosoa serikali, pamoja na kuziba mijadala mizito ndani ya Bunge.
Ingawa majina ya mwisho ya wagombea yataamuliwa na ngazi za juu za chama hicho, matokeo ya sasa yameweka uelekeo wa wazi kuwa sehemu kubwa ya wanachama wameonyesha hamu ya kuona sura mpya zikipewa nafasi ya uongozi.